Blog

Property International Ltd, ni kampuni ya kizalendo inayojishughulisha na Kupanga,Kupima na Kuuza viwanja katika maeneo mbali mbali ya ndani na nje ya jiji la Dar es salaam.
Property International Ltd ni moja kati ya wadhamini wa Mashindano ya 20 ya kuhifadhi na kusoma Qur an. Ambayo ni mashindano maalum yaliyoshirikisha Nchi kumi na nane kutoka barani Afrika,yaliyofanyika nchini Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya tarehe 19/05/2019, chini ya uangalizi wa Al Hikma Foundation.
Mbele ya Mh.Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Dr.John Pombe Joseph Magufuli.
Kijana wetu kutoka Tanzania visiwani,Ndg. Shamsuldin Hissein Bin Ally akaibuka kuwa mshindi wa tatu na kututoa kimasomaso watanzania.
Property International Ltd kwa kuunga mkono jitihada hizo wamemzawadia kijana huyo kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 1000, kilichopo maeneo ya kigamboni jijini Dar es salaam.
Katika picha Ndg.Ally Mbwana kutoka Property International ltd akimkabidhi nakala ya makubaliano juu ya zawadi ya kiwanja hicho wakati huohuo maandalizi ya rasimu ya hati ya kiwanja hicho yakiwa yanaendelea.